

Watu wengi wa dini tofauti wamekuwa wakibishana kuhusu dini na hata kuhusu YESU KRISTO NI NANI ? Hoja je ? YESU NI MUNGU ? YESU NI MWANA WA MUNGU? Je MUNGU Kwani Anazaa ? MAJIBU YESU NI NANI ? Tuangalie kwanza andiko la Luka 1:30-35 Malaika amtokea Mariam akamuambia usiogope Mariamu kwa maana umepata Neema kwa MUNGU,tazama utachukua mimba na kuzaa mtoto Mwanamume,na jina lake utamwita YESU huyo atakuwa mkuu ataitwa # Mwana wa alie Juu ,na Bwana MUNGU atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake,ataimiliki nyumba ya Yakobo na ufalme wake utakuwa hauna mwisho Mariamu akamuambia Malaika litakuwaje neno hilo maana sijui mume Malaika akamjibu akamuambia ,Roho Mtakatifu atakujulia juu yako na nguvu zake alie juu zitakufunika kama kivuli kwasababu hio Hicho kilicho zaliwa kitaitwa kitakatifu,#Mwana wa mungu
* JE MUNGU Anazaa kwanini yesu ni mwana ? MAJIBU Andiko la Yohana 3:6 kilicho zaliwa kimwili ni mwili na kilicho zaliwa kiroho ni Roho . Yesu amezaliwa kiroho.
* JE KUMUITA YESU NI MUNGU NI KOSA ? MAJIBU Waraka wa kwanza wa yohana 5:8 maana wapo watatu washuhudiao mbingu BABA(Yehova Mungu) NENO (Yesu kristo mwana wa Mungu baba,,Yoh 1:1-5) na ROHO Mtakatifu na watatu hawa ni umoja Andiko la pili lisisitizalo hawa ni umoja Yohana 10:30 mimi na baba tu umoja Andiko lingine lisibitishalo yesu na mungu hawatengani Yohana 14:8-10 filipo amuambia YESU bwana tuonyeshe baba yatutosha YESU akamuambia mimi nimekuwa pamoja nanyi siku zote wewe usinijue,? Alie niona mimi amemuona Baba basi wewe wasemaje tuonyeshe Baba ? Husadiki yakwamba mi ni ndani ya baba na baba yu ndani yangu ? Haya maneno niwaambiayo mimi sisemi kwa shauri langu: Lakini Baba akaae ndani yangu huzifanya kazi zake. Andiko la tatu lisibitishalo hawa hawatengeni Mwanzo1:26 Mungu asema natumfanye mtu kwa mfano wetu. Kwa maandiko hayo nazani nitakuwa nimeeleweka #ILANI Usikashifu wala kutukana imani ya watu wengine kama ujui chochote kuhusu imani yao kwani hupambani na waaminio imani hio bali mnapambana na Alie Juu alie Waita ktk Imani hiyo MUNGU Wa Kweli na Wapekee YEHOVA. Asanteni kwa maoni na maswali ni hapa,0766549742 na 0629051841.-Mt:Mabula
0689167646-Shukuru(Mhariri).
Ahsante Na Mungu Akubariki.