![]() |
Advertisement |
Usisahau ku Subscribe/Like&Share...https://youtu.be/Rc-I8Monfe4
Deuteronomy 11:2-7
Nanyi leo jueni; kwa kuwa sisemi sasa na vijana vyenu, ambao hawakujua, wala hawakuona adhabu ya BWANA, Mungu wenu, ukuu wake, na mkono wake wa nguvu, na mkono wake ulionyoka,
na ishara zake, na kazi zake alizomfanya Farao mfalme wa Misri, na nchi yake yote, katikati ya Misri;
na alivyolifanya jeshi la Misri, farasi zao, na magari yao; na alivyowafunikiza maji ya Bahari ya Shamu walipokuwa wakiwaandamia, na alivyowaangamiza BWANA hata hivi leo;
na mambo aliyowafanyia ninyi barani, hata mkaja mahali hapa;
na alivyowafanya Dathani, na Abiramu, wana wa Eliabu mwana wa Reubeni; nchi ilivyofunua kinywa chake, ikawameza, na walio nyumbani mwao, na mahema yao, na kila kitu kilichokuwa hai kikiwafuata, katikati ya Israeli yote;
7.lakini macho yenu yameiona kazi kubwa ya BWANA aliyoifanya, yote.
Hapo tunaona Mungu anaeleza anawambia wana wa Israel yakwamba wao wenyewe wanajua jinsi Mungu alivyowatoa Misri kwa Mkono wenye nguvu,maana haikua jambo la kawaida kuchomoka kwa Farao mfalme,aliekua katili na mwenye kujichumia faida kupitia wao waisraeli wenyewe,na waliishi misri kama watumwa.
Sasa Mungu anawakumbusha hvyo wajue yakua yeye Mungu ndie Ushindi wao kwamba Mungu tu ndie aliye watoa utumwani,haijalishi waliyopitia na walifanya nini,Ila tu wajue ni kwa Mkono wa BWANA yote yamefanyika na ni mpango wa BWANA(Unajua mpendwa wa Mungu kuna wakat mtu anapopitia wakati fulani anasahau kua ni Mungu ametenda,wakati mwingne anakana kabisa,ila Mungu anaweza kukushindia ktk mambo mengi na asikudai kumdhihirisha ili akuone utajitukuza wewe ama utamkumbuka matendo yake).
Sasa hapa hadi anasema Hasemi na Vivijana vyao!(yaani vijana wanaweza kuchukulia ni mzaha na story tu maana wengine hawakuona wanaskiaga tu kwamba Mungu alivyowatendea baba zao),ndio hapa anasema anazungumza na wao wenyewe walio jionea Ukuu wa Mungu, na kwa macho yao na wameona kweli Mungu ametenda na anaweza kutenda,
wamepigana vita,wamepita pengi ila Mungu pekee ndie Ushindi wao.
Ndugu mpendwa unaweza ukaona ni Story wewe unaeskia Leo habari hizi lakini nataka nikuambie habari njema leo,kua Ukimtegemea Mungu Mungu nae anatenda,anakushindia kwenye mambo makubwa magumu usiyo dhani,tena na kwa macho yako mwenyewe utaona!
Mi nikwambie ujapopita kwenye wakati mgumu wewe usibabaike,Aliyekuumba yu hai na mizigo ya shida zako anajua yeye,yanini kumtumaini mwanadamu!,Mungu alipomtoa mwanae afe kwaajili yako alikusudia,ndio mana unapaswa upeleke mizigo yote kwake na si kwa wanadamu,Maana ikiwa mshahara wa dhambi ni mauti,dhambi ndie iletayo adhabu,taabu n.k sasa je,mwanadam atakufutia dhambi?
ikiwa hafuti dhambi,je ushindi wako utatoka wapi?!.mtu asikubabaishe Msikilize Mungu,Ikiwa anakuita ktk Kristo uje utue mizigo yako iliosababiswa na dhambi,njoo kwake,duniani tunakosea mara nyingi sana,sisemi kila siku bali karibu kila saa,kwahiyo bila NEEMA YA MUNGU KUTUPATIA YESU,sisi tungeangamia sote maana ni wakosaji na sheria inatuhukumu,Ila Mungu kwa kutupenda Biblia inasema kaona vyema Keisto mwanae awe mtetezi wetu,asimame kwaajili yetu,
Bwana Yesu asifiwe sana,ikiwa kuna mtu anadani kusimama kwa haki yake mwenyewe,kwamba ati anatimiza sheria zote wala hatendi dhambi na aseme sasa kua Kristo si kitu kwake.Lahasha kama sivyo basi Sisi sote Tujue yakua MWOKOZI YESU NDIYE USHINDI WETU,
Acha vipofu wanaojidai hawaoni matendo makuu ya Mungu ndani ya Yesu wafuate akili zao,wanatukuza miungu waliojifanyia,wanabaki kusujudia watu na mashirika mbalimbali wakidhani yana msaada kwao wanasahau dhambi ipo,yote ni bure bila Yesu awezae kutakasa kwa Damu yake iliemwagika msalabani, Nafurahi kwasababu Mungu aliye hai yupo,Amemuweka kristo leo mbele yako kama alivyo muweka Musa Mbele ya wana wa Israel,Ananaka akusaidie,Awe Ushindi wako kwakua Umemwamini na kumtumainia.
...
Usiwajali wanaopita njia za mkato,alafu wanakucheka wewe wanakuona unachelewa na Mambo ya Mungu,usijali uonapo maadui zako wanajipanga kupigana na wewe usihofu ,yupo Mungu,Shikilia Tumaini lako,hata ujapopita katikati ya uvuli wa bonde la mauti yeye yupo upande wako.Anakuandalia kufurahi sio na rafiki zako tu anasema anaandaa meza mbele ya adui zako(yaani wao wenyewe adui zako watakuja wakitaka kula na wewe chakula) Halelujah
Me Nakukaribisha ktk video Hii imeandaliwa na Mtumish wa Mungu Mwinjilisti Paul Nkohozi akiwa Arusha ktk huduma yake ya Utume.
Me nasema Mungu ambariki maana amebeba Neno la Mungu moyoni mwake ili kutimiza kusudi la Mungu.
Mimi ni Shukuru Clement Blogger na Publisher wa Channel ya BIBLE4ALIFE
Sote tuifanye kazi ya Mungu kwa karama mbalimbali alizotupatia,
nasema Karibu tujifunze na Mungu wa mbinguni Akubariki.Ahsante.
Usisahau ku Subscribe/Like&Share...https://youtu.be/Rc-I8Monfe4
0 comments:
Unaweza kunipata kwa nambari 0689167646