Friday, May 17, 2019

ad300
Advertisement
Blog Hii Inahusu Kujifunza Neno La Mungu(Biblia),
Zaidi Sana Ikihusiamanisha Myenendo yetu ya  Maisha ya Kila siku na BIBLIA.
(kama ilivyo andikwa ktk Biblia 2Timoth 3:16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki
17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema).
..
Kwa Maana Hiyo Lengo na Kusudi Hasa ni Neno la Mungu Litusaidie Kuishi Maisha Sahihi(matakatifu)ya Kumpendeza yeye MUNGU ALIYE TUUMBA,
na kuishi vema sisi kama wanadamu.
(luka 2:52 Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.)
kumbuka;17 ili mtu wa Mungu awe kamili, tunaambiwa amekamilishwa(amekamilishwa na Neno la Mungu)apate kutenda kila tendo jema sawasawa na mpango wa Mungu.

ni fursa yako sasa kutumia vema wakati huu,Tujifunze tupate kuijua KWELI nayo KWELI ipate kutuweka Huru.
  Napenda kuwajulisha Wapendwa wasomaji kua nina kiu ya watu kumjua Mungu,tena ninapo Post Masomo haya ya injili kwanza namuomba Mungu na kuwaombea wote mnaopata bahati ya Kufikiwa na Mafundisho haya pia kua Kristo Awajalie Roho wake mpate kuelewa sana na yawafaeni kwa kadiri ya kipimo ili Mungu Wa Mbinguni Atukuzwe.

 Mathayo 11:29-30 27 Akasema, Nimekabidhiwa vyote na baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.
28-30 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.

KARIBU SANA TUJIFUNZE NA MUNGU WA MBINGUNI ATAKUBARIKI.AMINA.
.....KARIBU YOUTUBE PIA KWA MASOMO MBALIMBALI YA LIVE NA SAUTI
ANDIKA BIBLE4ALIFE AU FUATA LINK HAPA CHINI;
https://www.youtube.com/channel/UCPF1PjNxuPUENRlbtAYX4GA
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments:

Unaweza kunipata kwa nambari 0689167646