Tuesday, May 21, 2019

YESU KRISTO NDIYE USHINDI WETU



Usisahau ku Subscribe/Like&Share...https://youtu.be/Rc-I8Monfe4

Deuteronomy 11:2-7
Nanyi leo jueni; kwa kuwa sisemi sasa na vijana vyenu, ambao hawakujua, wala hawakuona adhabu ya BWANA, Mungu wenu, ukuu wake, na mkono wake wa nguvu, na mkono wake ulionyoka,
na ishara zake, na kazi zake alizomfanya Farao mfalme wa Misri, na nchi yake yote, katikati ya Misri;
na alivyolifanya jeshi la Misri, farasi zao, na magari yao; na alivyowafunikiza maji ya Bahari ya Shamu walipokuwa wakiwaandamia, na alivyowaangamiza BWANA hata hivi leo;
na mambo aliyowafanyia ninyi barani, hata mkaja mahali hapa;
na alivyowafanya Dathani, na Abiramu, wana wa Eliabu mwana wa Reubeni; nchi ilivyofunua kinywa chake, ikawameza, na walio nyumbani mwao, na mahema yao, na kila kitu kilichokuwa hai kikiwafuata, katikati ya Israeli yote;
7.lakini macho yenu yameiona kazi kubwa ya BWANA aliyoifanya, yote.

Hapo tunaona Mungu anaeleza anawambia wana wa Israel yakwamba wao wenyewe wanajua jinsi Mungu alivyowatoa Misri kwa Mkono wenye nguvu,maana haikua jambo la kawaida kuchomoka kwa Farao mfalme,aliekua katili na mwenye kujichumia faida kupitia wao waisraeli wenyewe,na waliishi misri kama watumwa.
Sasa Mungu anawakumbusha hvyo wajue yakua yeye Mungu ndie Ushindi wao kwamba Mungu tu ndie aliye watoa utumwani,haijalishi waliyopitia na walifanya nini,Ila tu wajue ni kwa Mkono wa BWANA yote yamefanyika na ni mpango wa BWANA(Unajua mpendwa wa Mungu kuna wakat mtu anapopitia wakati fulani anasahau kua ni Mungu ametenda,wakati mwingne anakana kabisa,ila Mungu anaweza kukushindia ktk mambo mengi na asikudai kumdhihirisha ili akuone utajitukuza wewe ama utamkumbuka matendo yake).

Sasa hapa hadi anasema Hasemi na Vivijana vyao!(yaani vijana wanaweza kuchukulia ni mzaha na story tu maana wengine hawakuona wanaskiaga tu kwamba Mungu alivyowatendea baba zao),ndio hapa anasema anazungumza na wao wenyewe walio jionea Ukuu wa Mungu, na kwa macho yao na wameona kweli Mungu ametenda na anaweza kutenda,
wamepigana vita,wamepita pengi ila Mungu pekee ndie Ushindi wao.

Ndugu mpendwa unaweza ukaona ni Story wewe unaeskia Leo habari hizi lakini nataka nikuambie habari njema leo,kua Ukimtegemea Mungu Mungu nae anatenda,anakushindia kwenye mambo makubwa magumu usiyo dhani,tena na kwa macho yako mwenyewe utaona!

Mi nikwambie ujapopita kwenye wakati mgumu wewe usibabaike,Aliyekuumba yu hai na mizigo ya shida zako anajua yeye,yanini kumtumaini mwanadamu!,Mungu alipomtoa mwanae afe kwaajili yako alikusudia,ndio mana unapaswa upeleke mizigo yote kwake na si kwa wanadamu,Maana ikiwa mshahara wa dhambi ni mauti,dhambi ndie iletayo adhabu,taabu n.k sasa je,mwanadam atakufutia dhambi?
ikiwa hafuti dhambi,je ushindi wako utatoka wapi?!.mtu asikubabaishe Msikilize Mungu,Ikiwa anakuita ktk Kristo uje utue mizigo yako iliosababiswa na dhambi,njoo kwake,duniani tunakosea mara nyingi sana,sisemi kila siku bali karibu kila saa,kwahiyo bila NEEMA YA MUNGU KUTUPATIA YESU,sisi tungeangamia sote maana ni wakosaji na sheria inatuhukumu,Ila Mungu kwa kutupenda Biblia inasema kaona vyema Keisto mwanae awe mtetezi wetu,asimame kwaajili yetu,

Bwana Yesu asifiwe sana,ikiwa kuna mtu anadani kusimama kwa haki yake mwenyewe,kwamba ati anatimiza sheria zote wala hatendi dhambi na aseme sasa kua Kristo si kitu kwake.Lahasha kama sivyo basi Sisi sote Tujue yakua MWOKOZI YESU NDIYE USHINDI WETU,

Acha vipofu wanaojidai hawaoni matendo makuu ya Mungu ndani ya Yesu wafuate akili zao,wanatukuza miungu waliojifanyia,wanabaki kusujudia watu na mashirika mbalimbali wakidhani yana msaada kwao wanasahau dhambi ipo,yote ni bure bila Yesu awezae kutakasa kwa Damu yake iliemwagika msalabani, Nafurahi kwasababu Mungu aliye hai yupo,Amemuweka kristo leo mbele yako kama alivyo muweka Musa Mbele ya wana wa Israel,Ananaka akusaidie,Awe Ushindi wako kwakua Umemwamini na kumtumainia.
...
Usiwajali wanaopita njia za mkato,alafu wanakucheka wewe wanakuona unachelewa na Mambo ya Mungu,usijali uonapo maadui zako wanajipanga kupigana na wewe usihofu ,yupo Mungu,Shikilia Tumaini lako,hata ujapopita katikati ya uvuli wa bonde la mauti yeye yupo upande wako.Anakuandalia kufurahi sio na rafiki zako tu anasema anaandaa meza mbele ya adui zako(yaani wao wenyewe adui zako watakuja wakitaka kula na wewe chakula) Halelujah

Me Nakukaribisha ktk video Hii imeandaliwa na Mtumish wa Mungu Mwinjilisti Paul Nkohozi akiwa Arusha ktk huduma yake ya Utume.
Me nasema Mungu ambariki maana amebeba Neno la Mungu moyoni mwake ili kutimiza kusudi la Mungu.

Mimi ni Shukuru Clement Blogger na Publisher wa Channel ya BIBLE4ALIFE
Sote tuifanye kazi ya Mungu kwa karama mbalimbali alizotupatia,
nasema Karibu tujifunze na Mungu wa mbinguni Akubariki.Ahsante.

Usisahau ku Subscribe/Like&Share...https://youtu.be/Rc-I8Monfe4

Friday, May 17, 2019

Blog Hii Inahusu Kujifunza Neno La Mungu(Biblia),
Zaidi Sana Ikihusiamanisha Myenendo yetu ya  Maisha ya Kila siku na BIBLIA.
(kama ilivyo andikwa ktk Biblia 2Timoth 3:16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki
17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema).
..
Kwa Maana Hiyo Lengo na Kusudi Hasa ni Neno la Mungu Litusaidie Kuishi Maisha Sahihi(matakatifu)ya Kumpendeza yeye MUNGU ALIYE TUUMBA,
na kuishi vema sisi kama wanadamu.
(luka 2:52 Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.)
kumbuka;17 ili mtu wa Mungu awe kamili, tunaambiwa amekamilishwa(amekamilishwa na Neno la Mungu)apate kutenda kila tendo jema sawasawa na mpango wa Mungu.

ni fursa yako sasa kutumia vema wakati huu,Tujifunze tupate kuijua KWELI nayo KWELI ipate kutuweka Huru.
  Napenda kuwajulisha Wapendwa wasomaji kua nina kiu ya watu kumjua Mungu,tena ninapo Post Masomo haya ya injili kwanza namuomba Mungu na kuwaombea wote mnaopata bahati ya Kufikiwa na Mafundisho haya pia kua Kristo Awajalie Roho wake mpate kuelewa sana na yawafaeni kwa kadiri ya kipimo ili Mungu Wa Mbinguni Atukuzwe.

 Mathayo 11:29-30 27 Akasema, Nimekabidhiwa vyote na baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.
28-30 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.

KARIBU SANA TUJIFUNZE NA MUNGU WA MBINGUNI ATAKUBARIKI.AMINA.
.....KARIBU YOUTUBE PIA KWA MASOMO MBALIMBALI YA LIVE NA SAUTI
ANDIKA BIBLE4ALIFE AU FUATA LINK HAPA CHINI;
https://www.youtube.com/channel/UCPF1PjNxuPUENRlbtAYX4GA

INJILI YA KRISTO.JE,UNAVYOSIKIA,UNAILELWA KUWA INJILI NI NINI?

 JE,UNAVYOSIKIA,UNAILELWA KUWA INJILI NI NINI?
Matthew 3:1-2
Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji AKIHUBIRI katika nyika ya Uyahudi, na kusema,
Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.
Ukisoma Mark 1:14 baada ya Yohana Yesu aliianza Injili nakusema hvohvo
Baada ya Yesu kupaa Mitume nae habar ni ileile Acts 2:38
Petro Awambia watu Tubuni Ufalme Wa Mungu Utawale kwenu.
..
INJILI Sio Kusema maneno yanayo wafurahisha watu,
INJILI sio Kutoa Misaada,
INJILI sio kumshawish mtu aend kanisani tu,
Injili sio Kumtabiria mtu utajiri.
Tena INJILI sio Kuponya watu tu na hata kama unabariki watu kwa Jina la Yesu,bado c injili.
kabla sijasema ni kwanini na kueleza injili zilizo tofauti kwanza napenda ujue Injili ni nini:
Injili sio kitu chochot kile ila INJILI NI HABARI NJEMA ZA UFALME WA MUNGU TU, (Ninapo sema Ufalme wa Mungu maana yake utawala wa Mungu,Serikali ya Mungu Mamlaka ya Mungu,Mtu anapo kuhubiria Injili maana yake anataka hayo Yakutawale Sio Baraka tu wala msaada wa mtu yeyote wala upako wake,hapana Ni Ufalme wa Mungu tu.
Maana hayo mahitaji yote c kitu ikiwa hujaruhusu Utawala wa Mungu kwako#Matthew 6:31-33
Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini,
Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa)
  KUSUDI LA INJILI:
WATU WATUBU NA KUBAATIZWA KTK KTK KRISTO WAWE KUNDI LA KRISTO
WAPATANE NA MUNGU.
HIYO NDIO INJILI, WATU WAPATE KUPOKEA MAISHA SAFI MAPYA NA SALAMA YALIYO KTK UFALME WA MUNGU.
INJILI YA KRISTO NI NEEMA YA MUNGU ILETAYO WOKOVU KWAKO KUPITIA KRISTO"YESU".(Warumi 1:16)
(Yani Msama wa dhambi,baraka na Uzima wa milele Vimo ktk Yesu,Na Ufalme wa Mungu Umefunuliwa ktk Yesu Kristo,kwahyo Injili ni lazma iwe inamlenga Yesu 100% na si ifuate mambo kama hayo nliotaj hapo awali kwamba kutimiza mahitaji ya watu kwa kutumia upako au uwezo ulionao,maana vitu bila Yesu hamna kitu,ni bure)
Natumai Umeelewa Injili ni nini.
Lakini sasa angalia Watu Wanaihubir injili kwa jinsi nyngne ya Ajabu kbsa dunia ya leo na ni kinyume na KUSUDI LA MUNGU,aidha Kwa kufuata tamaa zao za MALI au Kibinadam au kwa KUPOTEA kwao kulingana na Mapokeo yao kinyume na INJILI YA KRISTO.Na wana Sheria za Ajabu.
Ila Neno La Mungu Lina Tukumbusha na Kutufundsha kua kwa msisitizo Uliousikia ktk Injili tangu Yohana,Yesu Na Mitume Pia Manabii walitabiri Hyohyo habari Njema iletayo wokovu(Kristo),
(Soma Yoshua 1:7-8).
Bac Chunga Usje kupotezwa na Injili za Ki Ongo Fuata Meno La Mungu,Ni Silaha hiyo na ni habari njema Maana Ukiiacha Habari Njema Ulioisikia mwanzo Umepotea na kwa  Anaepotosha pia itakupasa Hukumu.(Galatians 1:9)
Usje uka skia mtu anasema njoo hapa Utapona au nenda pale ati Yesu Yupo alafu anasema anahubir ndio injili hyo! mara anasema Njoo Yesu yuko hapa?.Hapana,huyo ni mwongo!
labda hyo ni injili yake na sio ile iletayo WOKOVU,kwa hyo anapotosha.
itamfaa nini mtu kuombewa Apone ugonjwa au atajirike au apone alafu afe ktk dhambi(hajaacha dhambi wala kubatizwa,hajaruhusu mungu amtawale hana Neema) zitakua habari njema kwake kweli!! au ni habari njema kwakua ametajirika tu na kuepuka umaskini ila Sio kupata Wokovu maana Ufalme wa Mungu haupo ktk vitu,Na Sijaona mtu ukiwa tajiri siotu sijaona uende mbinguni bali hata uhakika wa kua na Amani sijaona kwa mtu tajiri tu.
Hivyo Kupokea Muujiza Sio Kupokea Ufalme Wa Mungu.
     Kwa Ushuhuda, Muulize Yuda alie kula mikate akaona na Miujiza!,tena mimi naona muujiza mkubwa ni kwa yuda,yeye licha ya kuona mambo mengi Yesu aliyotenda alimskia Yesu akisema Kuna mtu kati yenu atanisaliti(na niyeye)alafu Yuda anaskia na Anajijua ana wazo baya ila hataki kugeuka.
kama injili ingekua ni Muujiza na ishara Yuda angepona.Maana Mikate alikula=(Muujiza huo),
Na Kubaatizwa alibaatizwa ni ishara na alifuatisha nyingi tu.Lakini Kumbe Moyoni Mwake Sivyo Alivyo ipokea INJILI YA KRISTO,Maana Kumtii Yesu ni Kupata vyote.
Mpendwa Ufalme wa Mungu bhana pale ambapo wewe unaiskia Injili unampokea kwa njia ya Imani na kumkiri kwa kinywa Chako,Unakua Mpya ndani ya Yesu Unapobaatizwa ktk yeye naye Anakaa kwako daima,na baraka tele zikikufuata.
Mungu Wa Mbinguni Atusaidie Sana, maana ikiwaMungu upo ktk kumpokea Yesu,Yesu anabisha kwa njia ya Injili(kuhubir injil ni kubisha hodi kwa mtu afungue Moyo wake Yesu aingie)sasa Ikipotoshwa inaachwa kazi ya kristo inafanywa kazi ya watu wengne na si kuhubir injili sahihi?!
Kila Anae Hubiri Injili ni lazima alenge Yesu na Wokovu wake ikiwa anadai ni Injili ya Kristo.
Nimalizie;
Mark 16:15-16(Yesu asema)
Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.
Matthew 28:18-20(tena)
Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.Amina
Mungu Wa Mbinguni Awalinde na kutubariki Sana.
..Unaweza kushare mpendwa Injili ni ya wote..

Thursday, May 10, 2018

Thursday, May 3, 2018

EPUKA LAANA "USIMSEME VIBAYA MTU"


Mhubiri:7.20 Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi. .. YESU APEWE SIFA. Sina Maana ya KuSapoti Maovu,Wala Haimaanishi Kukosea Ni Muhimu,"Hapana" Ila Niseme Neno La Msingi Sana #Ni_Juu ya Wanaowahukumugi Watumishi Wa Mungu na Kusema Kwamba Ni Waovu. ..Ndio Wapo Watumish Waovu,Ambao Hawamtumikii Mungu Wa Kweli,(YEHOVA MUNGU ALIYE JUU). ,,,Lakini Hapa Nasema Kwa Watumish wa Kweli Wa MUNGU KWELI. Sasa Watu Wengi Wamekua Wakiwahukumu Watu hao Walio Mpokea Yesu(Kuanzia Wachungaji,Na Watu wengne Waliomkiri Na Wamemkubali Kua Ndie Alietumwa Na Mungu Kwa Ajili Ya Kuwa Okoa Wanadamu/Masihi/Na Wanaamini Wataokolewa na Kuachana na Dhambi)(Ni Kweli Kabisa) Wapendwa Hawa Wa Mungu Kwa Jina Lingne Wanaitwa "Walokole" Leo Hii Hawaishi Kwa Amani,Wamekua Wakisemwa Ni Waovu, Watu Wengne Huwachukia Na Kuwasengenya. Wakisema "Mlokole Gani,Yuko Hivi/Vile Mara Hafanyi Kile,Mara Tumemchoka Na Hichi. Jamani!! Mtu Yupo Duniani Hayupo Mbinguni,Tena Ninyi Wenyewe Ndio Mmekua Jaribu Kwake Maana Hawaishi Kumtega Na Kuwa Sababu Ya Kukosea Kwake Mtumishi,Licha Ya Maisha Ya Dhambi Yaliotawala Duniani Ambayo Ndio Majaribu Makubwa. .. Watumish wa Mungu Wanajitahd Kutenda Mema kwa Msaada Wa Mungu,Ila Watu Hawaoni Wao Ni Kuhesabu Makosa tu. ..Sasa Wewe Ni Nani Hata Umhukumu Mtu Wa Mungu? ..Yeye Ndio Anajua Anachokifanya Na Mungu Wake,Na Hukumu Yake Anayo Mungu. ,,Paulo Mtume Alisema, Kama ningekua natafuta kuwapendeza wanadam nisingekua mtumishi wa Kristo Galatia 1:10 Ndivyo ilivyo na Watumish wote Wa Mungu,Hata hivyo Hawajatumwa kuwapendza Watu wametumwa kuwaokoa,Kuwaambia Yesu Ni BWANA(Wamwamini Masihi) Ila wengne Hata Ujumbe wa Mungu kwao ni Chukizo. ..Sasa Usijitaftie Laana. Epuka Kumnenea Neno Baya Mtu Wa Mungu. Ww Ikiwa Umeona Hutaki Mambo Ya Kumcha Mungu,Uko Bize Na Dhambi,Usiwe Mwalimu Wa Kumlaumu Mwenzio Nakati Ww Unakosea, Umesahau Wale Waliokua Wakitaka Kumhukumu Yule Mama Aliefumaniwa kule Galilaya?! Wakamleta Mbele Ya Yesu Wamuhukumu,Yesu Akawambia Ikiwa Kunamtu Hajawah Tenda Dhambi Awe Wa Kwanza Kumpiga Mawe(maana Sheria ya Wakat ule mtu Akifumwa amezini na Mke/Mume wa Mtu Ni Apigwe mawe Hadi Kufa)(Yoh 8:3-7) Bac Mwache Mwenzio Ambae Akikosea Anajua Atamlilia Mungu wake Kwani Anatambua Dhambi Ni Uasi Kwa Mungu na Huwa Hawatendi kwa Makusudia Maana mafundisho Ya Mungu kupitia Kristo yanawaepusha a Kuwaongoza. Na kua Mtakatifu Sio kwamba Hawatend Dhamb kbsa Bali Roho Wa Mungu Huwasaidia Pia Pale Waangukapo Hutakaswa Kwa Kuomba Toba maana Sio Kusudi Lao. Luke 17:1 Akawaambia wanafunzi wake, Makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake! ,,Hii Inamaana Kuna Makosa Ya Kudhamiria/Yakuzoea Ndio Mungu Hapendi Maana Ni Yakukubali mtu mwenyewe kumwasi Mungu Kwa Hiari Yake Na Si Kuteleza.(alafu weng husingizia kuteleza nakati wanadhamiria,ni dhambi) Ok Kwahyo Usifkirie Kazi Ya Mlokole Au Mchungaji Ni Kuona Anakufanyia Mematu. Hata Yesu Hakuwa Pendeza Wote Inamaana Hakua Mtakatifu? ,,Petro Nae Alimkana hadi Yesu Mwenyewe(Kwa hofu ya kuuawa na wayahudi) Lakini baadae alitubu naku Rejea, Je,Nae Pia Hakua Mlokole? ,,Nawaambia Watu Wa Namna hii,wa kuhukumuhukumu, Msipo Tubu na kuacha,Yatawaletea Madhara. Jaribu kufikiri,Mtume Paulo Alietumwa Na Kristo na Si Mwanadam Alipoona Amemnenea Vibaya Annania Kuhani Mkuu(Mchungaji Kiongozi) bila Kujua Alitubu UPESI,(Matendo Ya Mitume 23:5 Paulo akajibu, “Ndugu zangu, sikujua kwamba yeye ni kuhani mkuu. Kwa maana Maandiko yanasema, ‘Usimseme vibaya kiongozi wa watu wako.) ..Tubu Leo Ndugu Na Uache Dhambi. Maana Mungu Mwenyewe Ndie Amekataza Tabia Hyo Ya Kunena Na Kuhukumu Mabaya Unayoyaona Kwa Watumishi. ..Mungu Awabariki.Nawapenda Pia. Image may contain: one or more people and people standing Image may contain: 1 person, sitting and shoes